BERLIN: Serikali ya mseto mkuu kuundwa Ujerumani ?
26 Septemba 2005Matangazo
Mwenyekiti wa chama cha CDU bi Angela Merkel amekitaka chama cha kansela Schröder SDP kuacha kudai kiti cha ukansela ili kuwezesha kufanyika mazungumzo juu ya kuunda serikali ya mseto baina ya vyama vikuu vya siasa hapa nchini Ujerumani.
Hatahivyo bi Merkel amesisitiza kwamba kutokana na wingi wa kura chama chake kina haki ya kudai uongozi wa serikali.
Ujerumani kwa sasa inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu wa hivi karibuni ambapo hakuna chama kilichofanikiwa kupata kura za kutosha ili kuunda serikali peke yake.
.