BERLIN: Sera za serikali ya Merkel zafanikiwa
21 Agosti 2006Matangazo
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema sera za serikali yake zimeanza kuonyesha mafanikio baada ya uongozi wa miezi tisa.Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin,Merkel alizungumza pia juu ya utaratibu wa amani katika Mashariki ya Kati.Amesema,makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hezbollah yalio nyeti,yasitiwe hatarini.Akasisitiza kuwa ni muhimu kwa Ulaya kushiriki katika jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.Lakini masharti ya vikosi hivyo yapaswa kuandaliwa na kukubaliwa na serikali ya Lebanon.Na kuhusu siasa za ndani Merkel amesema serikali yake mwakani bado inatazamia kupandisha kodi ya ongezeko la thamani ya bidhaa kwa asilimia 3,lakini kodi zingine hazitoongezwa.