BERLIN: Schäuble amesifu matokeo ya mkutano
28 Septemba 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble ameliambia bunge mjini Berlin,mkutano uliofanywa siku ya Jumatano kati ya viongozi wa serikali na wa jumuiya ya waislamu wanaoishi nchini Ujerumani umekuwa na mafanikio.Amesema, licha ya majadiliano hayo kuwa magumu,mkutano huo ulifanikiwa kuwaeleza Wajerumani na hata Waislamu kuwa jumuiya ya waislamu pia tangu muda mrefu ni sehemu ya jamii na sio wageni.Majadiliano hayo ni mwanzo wa mazungumzo yatakayoendelea kufanywa kwa muda wa miaka miwili ijayo kati ya serikali na wajumbe wa jumuiya ya waislamu nchini Ujerumani.