Berlin. Rais wa Ujerumani sasa kuamua juu ya uchaguzi wa mapema nchini humo.
2 Julai 2005Uamuzi wa iwapo wapiga kura wa Ujerumani watafanya uchaguzi mkuu mwaka mmoja kabla ya muda wake sasa uko katika mikono ya rais Horst Köhler.
Rais Köhler sasa atakuwa na wiki tatu za kutoa uamuzi iwapo kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi , kutokana na kura iliyopigwa jana Ijumaa bungeni ya kutokuwa na imani na kansela .
Kansela Gerhard Schröder alipanga kushindwa kura hiyo , na amepata kile alichokitaka , wakati wajumbe kadha wa muungano wake wa serikali walipoacha kupiga kura.
Bwana Schröder awali alitangaza nia yake ya kutaka kufanyika kwa uchaguzi na mapema mara tu baada ya chama chake cha Social Democrats kushindwa vibaya katika uchaguzi wa jimbo muhimu la North Rhine Westphalia mwezi wa May.