Berlin. Rais wa Ujerumani aisifu China.
11 Novemba 2005Rais wa Ujerumani Horst Köhler amesifu hatua za maendeleo zilizopigwa na China za kufungua milango yake kwa mataifa yote duniani.
Kufuatia mkutano na rais wa China Hu Jintao ambaye anaizuru Ujerumani , rais Köhler amesema kuwa China imefanikiwa mno katika miongoni michache iliyopita.
Lakini pia amedokeza kuwa China inapaswa kujitahidi zaidi , akisema kuwa haja ya watu kuishi katika uhuru na heshima ni suala la lazima.
Viongozi hao wawili pia wamehudhuria sherehe ya kutiwa saini kwa makubaliano yenye gharama ya Euro bilioni 1.3 ambapo kampuni la Siemens la Ujerumani litatoa treni 60 ziendazo kasi nchini China.
Leo Ijumaa , Hu anatarajiwa kukutana na kansela anayeondoka madarakani Gerhard Schröder na kansela mteule Angela Merkel .