BERLIN. Rais wa Israel azuru Ujerumani.
31 Mei 2005Matangazo
Rais Moshe Katzav wa Israel anazuru Ujerumani kuadhimisha miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Ujerumani na Israel.
Rais Katzav na mwenyeji wake rais Horst Koehler wa Ujerumani wamesema kuwa nchi hizi mbili zitaanzisha mfuko maalumu wa fedha wa kumbukumbu ya wahanga wa mafashisti wa kinazi zitakazo tumiwa kuwaendeleza vijana katika mawasiliano,sayansi na usanii katika nchi hizi mbili.
Rais Katzav ameipongeza Ujerumani kwa ukomavu wake wa kupambana na siasa isiyo na kadiri.