BERLIN Rais wa Israel ahutubia bunge la Ujerumani
31 Mei 2005Matangazo
Rais wa Israel bwana Moshe Katzav ametoa mwito kwa kizazi cha leo wa kuzingatia mafunzo yanayotokana na maangamizi ya wayahudi barani Ulaya.
Bwana Katzav amesema ni muhimu kuchukua hatua thabiti za kupambana na chuki dhidi ya wayahudi inayoibuka tena.
Akilihutubia bunge la Ujerumani mjini Berlin leo, kiongozi huyo wa Israel ameeleza wasi wasi juu ya kuendelea kuota mizizi kwa ufashisti mamboleo katika jamii ya Ujerumani.
Bwana Katzav pia ametahadharisha kwamba kuwepo kwa waislamu wenye siasa kali pamoja na makundi ya itikadi kali ya milengo ya kushoto na kulia inapalilia chuki dhidi ya wayahudi barani Ulaya.