BERLIN : Rais wa China ziarani Ujerumani
12 Novemba 2005Matangazo
Rais wa China Hu Jintao aliyoko ziarani nchini Ujerumani amekutana na Kansela anayeondoka madarakani Gerhard Schroeder mjini Berlin.
Kufuatia mazungumzo yaoa Schroeder ameutumia mkutano na waandishi wa habari kuelezea uhusiano unaozidi kukuwa kati ya nchi hizi mbili.Viongozi hao wawili baadae waliweka jiwe la msingi kwa ajili ya Kituo kipya cha Utamaduni cha China mjini Berlin.
Awali Hu alikutana na Kansela mteule Angela Merkel ambapo imeelezwa kwamba mazungumzo yao yalidhibitiwa na masuala ya kutumia upya nishati na mazingira.