BERLIN: Rais Mbeki asifu mchango wa Ujerumani
9 Julai 2006Matangazo
Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini amesifu mchango wa Ujerumani wa kupeleka vikosi vyake kulinda usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.Baada ya kukutana na kansela Angela Merkel wa Ujerumani mjini Berlin,viongozi hao walikubaliana kuwa maendeleo nchini Congo na Sudan ni muhimu kwa amani na utulivu katika bara zima la Afrika.Vikosi vya Ujerumani ni sehemu ya vikosi vya kimataifa vitakavyolinda usalama nchini Congo wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanywa mwisho wa mwezi wa Julai.