BERLIN : Rais Köhl amsifu marehemu Rais Ford
28 Desemba 2006Rais Horst Köhler wa Ujerumani amemsifu Rais wa zamani wa Marekani Gerald Ford aliefariki dunia hapo jana kuwa ni Mmarekani mashuhuri alietumikia nchi yake wakati wa kipindi kigumu.
Ford mwenye umri wa miaka 93 amefariki hapo jana nyumbani kwake huko Carlifonia.Katika taarifa aliyotuma kwa Rais George W. Bush Köhler amesema Ford amefanya mengi kukuza uhusiano kati ya Marekani na Ulaya na pia alikuwa baba muasisi wa Kundi La Mataifa Manane yenye Maendeleo Makubwa ya Viwanda Duniani.
Ford alikuwa ni Rais pekee wa Maraekani ambaye alikuwa hakuchaguliwa na wananchi kwenye nyadhifa zote mbili za Urais na Makamo wa Urais.
Kufuatia kujiuzulu kwa Rais Richard Nixon kutokana na kashfa ya Watergate hapo mwaka 1974 mbunge huyo wa zamani alitumikia Urais wa 38 wa Marekani hadi hapo aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Urais na Jimmy Carter wa Chama cha Demokrat mwaka 1976.