BERLIN. Rais Hu Jiantao wa China ziarani Ujerumani
11 Novemba 2005Matangazo
Rais wa Shirikisho la jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler ameipongeza China kwa kufungua milango yake kwa jumuiya ya dunia nzima.
Rais Köhler alisema hayo mjini Berlin, katika mkutano na kiongozi wa China Hu Jintao ambae yumo ziarani hapa Ujerumani.
Hata hivyo rais Horst Köhler ameihimiza china kushughulikia zaidi maswala ya haki za binadamu.
Viongozi hao wawili walihudhuria kutiwa saini makubaliano ya Euro bilioni 1.3 yatakayo ihusisha kampuni ya Siemens ya Ujerumani kupeleka treni 60 za mwendo wa kasi nchini China.
Leo hii rais Hu Jintao atakukutana na Kansela wa Ujerumani anaeondoka Gerhard Schröder na kansela mteule bibi Angela Merkel.