BERLIN. Polisi yamkamata mtuhumiwa wa kuuza vifaa vya kutengezea makombora katika mataifa ya kigeni.
23 Mei 2005Matangazo
Polisi nchini Ujerumani imemtia mbaroni meneja wa kampuni moja anayetuhumiwa kwa kuyauzia mataifa ya kigeni vifaa vinavyotumiwa ketengenezea makombora.
Waongoza mashtaka hapa nchini wamesema kukamatwa kwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 46 kunafuatia kutiwa nguvuni kwa mkuu wa uuzaji wa bidhaa katika mataifa ya nje wa kampuni lililoko mkoani Thuringia, mashariki mwa Ujerumani mwezi uliopita.
Inasemekana kampuni hilo limekuwa likiyauzia mataifa ya kigeni vifaa hivyo kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.