BERLIN. Pasi mpya za kusafiria zatolewa nchini Ujerumani
2 Novemba 2005Matangazo
Serikali ya Ujerumani imenza zoezi la kutoa hati mpya za kusafiria zilizo tengezwa kwa teknolojia ya kisasa.
Hati hizo mpya zitakuwa na uwezo wa kielectroniki wa kudhibiti sura ya mwenye pasi kidijitali na itakuwa vigumu kughushi au kufanya udangayifu.
Ujerumani ni miongoni mwa nchi za kwanza kutumia aina hii ya teknologia ya juu katika maswala ya utambulisho.
Kwa sasa gharama za kuomba pasi za kusafiria nchini Ujerumani zitapanda kutoka Euro 29 hadi Euro 59.