BERLIN : Mzozo wa uongozi bado warindima
2 Oktoba 2005Vingozi wakuu wa chama cha kihafidhina CDU cha Angela Merkel na wale wa chama cha SPD cha Kansela Gerhard Schroeder hapo jana wametilia mkazo haki ya vyama vyao kwa wadhifa wanaougombania wa Ukansela kabla ya uchaguzi wa Dresden leo hii.
Wakati matokeo ya uchaguzi huo ambao uliahirishwa kutokana na kifo cha mgombea hayatobadili matokeo ya uchaguzi wa bunge wa Septemba 18 ambapo CDU wana wingi wa viti vitatu bungeni wengi wanatumai yatatuwa mzozo huo mkubwa wa uongozi.
Wolfgang Schaeuble naibu mkuu wa chama cha Christian Demokrat CDU amesisitiza katika matamshi yaliyochapishwa hapo jana na gazeti moja la Ujerumani kwamba pande hizo mbili hazina budi kufikia makubaliano haraka na kwamba mazungumzo na majadiliano hayawezi kuendelea milele.