Berlin. Mvua iliyoambatana na upepo mkali yaua tisa katika bara la Ulaya.
5 Julai 2005Matangazo
Siku kadha za mvua kubwa iliyoambata na upepo mkali katika eneo la bara la Ulaya imesababisha vifo vya watu tisa , na barabara kadha pamoja na madaraja yakiwa hayapitiki kwa kujaa maji.
Baadhi ya wahanga wamepigwa na radi.
Eneo lililoathirika zaidi ni Romania na Bulgaria , ambako maji yalizuwia reli kuelekea katika bandari ya bahari nyeusi ya Varna . Mafuriko yametenga maeneo kadha na watu hawawezi kutoka katika maeneo hayo.
Kumekuwa pia na mvua kubwa iliyoambatana na upepo nchini Uholanzi , Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani na Uswisi.