BERLIN: Munterfering ni naibu wa kansela wa Ujerumani
13 Oktoba 2005Matangazo
Mwenyekiti wa chama cha SPD Franz Munterfering, atakuwa naibu wa kansela wa Ujerumani kwenye serikali mpya ya muungano itayoongozwa na Angela Merkel. Munterfering anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo baada ya kansela Gerhard Schröder kuthibitisha hatoshiriki kwenye serikali mpya ya Merkel.
Frank Walter Steinmeir wa chama cha SPD ataichukua nafasi ya Joschka Fischer na kuwa waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Ujerumani. Gavana wa zamani wa mkoa wa Northrhine Westfalia, Peer Steinbrueck, atachukua nafasi ya Hans Eichel na kuwa waziri mpya wa fedha.
Heidermarie Wieczorek-Zeul ataendelea na wadhifa wake kama waziri wa misaada ya maendeleo. Wizara ya uchumi itaongozwa na mshiriki wa Merkel, Edmund Stoiber.