BERLIN: Munterfering kuwa naibu wa kansela
13 Oktoba 2005Matangazo
Mwenyekiti wa chama cha SPD Franz Munterfering, atakuwa naibu wa kansela wa Ujerumani kwenye serikali mpya ya muungano itayooongozwa na Angela Merkel. Munterfering anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo baada ya kansela Gerhard Schröder kuthibitisha hatoshiriki kwenye serikali itakayoongozwa na Merkel.
Frank Walter Steinmeir wa chama cha SPD atakuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani. Gavana wa zamani wa mkoa wa Northrine Westfalia, Peer Steinbrueck, atachukua nafasi ya Hans Eichel na kuwa waziri mpya wa fedha. Heidermarie Wieczorek-Zeul ataendelea na wadhifa wake kama waziri wa maeondeleo.