BERLIN: Mtaalamu wa maswala ya Mashariki ya kati afariki.
25 Februari 2005Matangazo
Aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati na mbunge wa Ujerumani Bwana Hans Jürgen Wischnewski amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Marehemu Wischnewski alikuwa mwanachama wa chama cha SDP na alikuwa mjumbe maalum wakati wa Makansela Willy Brandt na Helmut Schmidt.
Mwka wa 1977 alisaidia katika juhudi za kuwaokoa watu 90 waliotekwa nyara katika ndege ya shirika la Ujerumani, Lufthansa katika mji wa Mogadishu nchini Somalia.