BERLIN: Mkataba wa bomba la kusafirishia gesi
9 Septemba 2005Matangazo
Ujerumani na Russia zimetia saini makubaliano ya kujenga bomba la gesi kati ya nchi hizo mbili.Rais Vladimir Putin wa Russia na Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani walihitimisha makubaliano hayo ya Dola bilioni tano mjini Berlin.Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 1,200 na litaanzia karibu na mji wa St.Petersburg na kupitia chini ya Bahari ya Baltic hadi kaskazini-mashariki ya pwani ya Ujerumani.Bomba hilo litajengwa na makampuni ya Kijerumani ya E.ON na BASF pamoja na shirika kuu la nishati la Russia,Gazprom.Inatarajiwa kuwa bomba hilo la gesi litaanza kutumiwa mwaka 2010.Mkataba huo umekosolewa na Ukraine na Poland,ambazo hivi sasa hupokea ushuru wa mabomba ya Russia yanayopitia nchi hizo mbili.