BERLIN: Mkasa wa mwaka wa mauaji Ujerumani.
23 Machi 2005Matangazo
Mamia ya polisi wa Ujerumani wamo katika harakati za kuwasaka wahanga wa kile kilichotajwa kuwa mauaji ya mwaka.
Msako mkali umeanzishwa katika mji wa Bremerhaven sehemu za viwandani huko kaskazini mwa Ujerumani baada ya mfungwa mmoja mwenye uhusiano na Marc Hoffman, muhusika mkuu wa mauaji hayo kutoa taarifa kwa polisi kuwa Hoffman alikiri kuwa aliwauwa watu sita wakiwemo watoto wawili wenye umri wa miaka minane ambao ndio haswa chanzo cha yeye kufungwa.
Mfungwa huyo alieleza pia kuwa Hoffman amemuambia kuhusu mauaji ya watoto wengine wawili na wanawake wawili huko Ujerumani Mashariki.