BERLIN. Mgogoro wa visa nchini Ujerumani umeendelea kuwa mjadala mkubwa.
17 Februari 2005Matangazo
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na vyombo vya habari, waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, alijua ulegevu uliokuwa ukiendelea kuhusiana na kutolewa kwa visa hizo, kulikowaruhusu wahamiaji kutoka Ulaya mashariki kuingia nchini Ujerumani kuanzia mwaka wa 2000. Gazeti la Suddeutsche limesema Fischer alipuuza onyo kutoka kwa wanasiasa mashuhuri. Wabunge wa upinzani wa kikosavativ wanasema kulegeza sheria za utoaji visa kuliwasidia maelfu ya wahamiaji haramu kuingia Ujerumani wakitumia visa za watalii, wengi wao wakisaidiwa na makundi ya kigaidi. Tume ya bunge inayochunguza kashfa hiyo inatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza hii leo.