BERLIN : Merkel ataka utekelezaji wa azimio haraka
12 Agosti 2006Matangazo
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani hapo jana amelikaribisha azimo la Umoja wa mataifa lenye kutowa wito wa kukomesha umwagaji damu Mashariki ya Kati na amehimiza utekelezaji wa haraka na wa uthahibiti wa azimio hilo.
Kansela Merkel ambaye serikali yake imekuwa ikitowa wito wa kufikiwa kwa suluhisho la kidiplomasia tokea kuanza kwa mzozo huo uliodumu kwa mwezi mmoja kati ya Israel na Hizbollah amesema hio ni ishara muhimu ya azma ya jumuiya ya kimataifa kukomesha operesheni za kijeshi.
Ameongeza kusema kwamba sasa ni suala la kulitekeleza azimio hilo mara moja na kwa utahibiti bila ya kutaja iwapo jeshi la Ujerumani litashiriki katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.