BERLIN: Merkel akutana na Siniora
29 Septemba 2006Matangazo
Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel alisema jana jioni kwamba kikosi cha wanamaji cha Ujerumani katika fukwe za bahari ya Lebanon kitalisaidia jeshi la nchi hiyo kuilinda bahari na mpaka wake.
Aidha Merkel alisema jeshi la Ujerumani litasaidia pia kuzuia kuingizwa kwa silaha zinazonuiwa kupelekwa kwa wanamgambo wa Hezbollah.
Kansela Merkel aliyasemahayo wakati alipozungumza na waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora mjini Berlin. Merkel alisema Ujerumani inataka kuisadia Lebanon kujenga upya miundo mbinu yake na kuunda taifa lenye nguvu na demokrasia.