BERLIN: Mazungumzo juu ya kuunda serikali yafanyika
22 Septemba 2005Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani leo wanakutana na wajumbe wa vyama vingine vya siasa ili kuzungumzia mawezekano ya kuunda serikali ya mseto.
Viongozi wa vyama vya CDU/CSU wanatarajiwa kukutana na wajumbe wa vyama vya waliberali FDPna Kijani ili kutafakari mawezekano ya kuunda serikali .
Wawakilishi wa vyama hivyo vikuu vya upinzani pia watafanya mazungumzo na wajumbe wa chama cha SDP kwa lengo la kutafuta uwezekano mwingine wa kuunda serikali chini ya mseto mkubwa.
Ujerumani kwa sasa inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia matokeo ya uchaguzi wa mwishoni mwa iki iliyopita ambapo hakuna chama kilichoweza kupata kura za kutosha ili kuunda serikali.
Kila upande wa vyama vikuu ,SDP na CDU unadai uongozi wa serikali.
.