BERLIN. Mawakili wataka Meiwes afungwe maisha.
22 Aprili 2005Mawakili wa serikali nchini Ujerumani wametoa wito wa kusikizwa tena upya kwa kesi ya Armin Meiwes mjerumani anae tumikia kifungo cha miaka minane na nusu kwa kosa la kuua bila kukusudia baada ya kumuua na kumla mtu mwaka 2001.
Mawakili hao wanasema kuwa hukumu hiyo ni ndogo na badala yake Armin Meiwes anastahili kutumikia kifungo cha maisha.
Sakata hii imekuja baada ya mawakili wa Meiwes kukata rufani ya kutaka adhabu ya miaka minane ipunguzwe kwani Meiwes aliua bila kukusudia na la zaidi marehemu alikubali mwenyewe kuuwawa na kisha kuliwa.
Meiwes mwenye umri wa miaka 43 mtalaamu wa mitambo ya tarakilishi alimuua na kumla Bernd Juergen Brandes baada ya kutoa tangazo katika mtandao wa internet mwaka wa 2001 akitaka mtu ajitolee kuuwawa na kuliwa ambako Brandes aliitikia wito wa Meiwes na mauti yakamfika.